MAOMBI YA TOBA NA REHEMA π Zaburi 51:1–2 “Ee Mungu, unirehemu sawasawa na fadhili zako; Kwa wingi wa rehema zako, uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.” MAOMBI YA TOBA NA REHEMAπ§ Ee Baba wa mbinguni, Nakuja mbele zako kwa unyenyekevu mkubwa, nikiwa na moyo wa toba. Bwana, nakuomba unirehemu sawasawa na wingi wa fadhili zako. Nisamehe dhambi zangu zote — nilizozifanya kwa kujua na hata zile nilizozifanya bila kujua. Ee Mungu wangu, yamkini kuna mlango niliufungua kwa njia ya dhambi, mlango uliompa nafasi adui kuingia katika maisha yangu. Kwa jina la Yesu, ninatubu leo kwa dhati. Naomba unioshe kwa damu ya Yesu, unitakase kabisa na uovu wangu. Bwana, kila mahali nilipokosea, kila hatua niliyopotoka, naomba rehema zako zifute hatia yangu. Ee Mungu, ikiwa shetani ametumia udhaifu wangu kunirudisha nyuma, hasa kupitia ndoto za shule, kunizuia nisipige hatua, leo nasimama kinyume na hilo. Kwa mamlaka ya jina la Yesu, ninafunga kila mlango wa dhambi n...