Dunia itakunjwa Kama karatasi?

Jibu: Hakuna mstari wowote katika biblia takatifu unaosema kwamba dunia siku moja itakunjwa kama karatasi na kutupwa motoni. Mstari ambao unawachanganya wengi ni ule wa Isaya 34:4 unaosema..

Isaya 34:4 “Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, NA MBINGU ZITAKUNJWA KAMA KARATASI, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.”

Ukiisoma hiyo Isaya 34, utaona ni unabii wa Siku ya mwisho. Na katika huo mstari wa 4,  unabii unasema kuwa siku hiyo  “mbingu zitakunjwa kama karatasi”. Hapo anasema “mbingu” na si “nchi” au “ardhi” au “dunia”  bali mbingu!!. Hizo ndizo zitakazokunjwa kama karatasi… Na mbingu inayozungumziwa hapo sio ile Malaika watakatifu waliyopo, La!.. bali ni hii tunayoiona yenye nyota, mwezi na jua, na sayari.

Na hazitakunjwa kama karatasi na kisha kutupwa motoni!.. La! Maandiko hayajasema hivyo, yameishia tu hapo kusema kuwa zitakunjwa kama karatasi. Na kukunjwa kunakozungumziwa hapo sio kukunjwa  kwa kusokotwa sokotwa kama uchafu, hapana! Bali kukunjwa kama vile mtu anayekunja ngozi.

Sasa ili tuelewe vizuri zitakunjwaje kunjwaje siku hiyo kama karatasi, twende pamoja kwenye kitabu cha Ufunuo.

Ufunuo 6: 12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13  NA NYOTA ZIKAANGUKA JUU YA NCHI KAMA VILE MTINI UPUKUTISHAVYO MAPOOZA YAKE, UTIKISWAPO NA UPEPO MWINGI.

14  MBINGU ZIKAONDOLEWA KAMA UKURASA ULIVYOKUNJWA, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

15  Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

16  wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17  Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Umeona hapo?.. Katika siku ile ya mwisho, muhuri wa 7 utakapofunguliwa, wakati Yesu atakaporudi na watakatifu wake aliowanyakua. Siku hiyo, nyota zitaanguka, (maana yake zitaondolewa). Ghafla tu, watu watashangaa jua limezama wakati wa adhuhuri, na mwezi umekuwa mwekundu kama damu.. na juu nyota zinaanza kujikusanya pamoja na kuanguka..kama vile ukurasa (Yaani karatasi) linavyofunguliwa..

Tunaweza kulisoma tena jambo hilo vizuri katika kitabu cha Mathayo..

Mathayo 24:27  “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

28  Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

29  Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, NA NYOTA ZITAANGUKA MBINGUNI, NA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA;

30  ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”

Comments

Popular posts from this blog

BARAKA ZA BWANA

Pasaka/Easter✝️✅

CHRISTIAN RELATIONS BEFORE MARRIAGE๐Ÿ’๐Ÿ’Œ