BARAKA ZA BWANA

POKEA BARAKA ZA BWANA


Kuna aina tano(5) za baraka atoazo MUNGU kwa watu wake.

1. Baraka za afya.

2. Baraka za uchumi.

3. Baraka za ndoa.

4. Baraka za uzao.

5. Baraka za kutamalaki.


Baraka yake kutamalaki kwa jina lingine inaitwa Kumiliki na kutawala,  Sasa moja ya mamlaka ya Mteule wa MUNGU aliyeokolewa na Bwana YESU ni kumiliki na kutawala kwenye ulimwengu wa roho.

Tunamiliki na kutawala kwa sababu tuna mamlaka ya jina la YESU KRISTO.


Jukumu la kwanza tulilopewa wanadamu na MUNGU Muumba wetu ni kutawala.

Mwanzo 1:26-27 ''MUNGU akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; WAKATAWALE samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.


MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba''

Kwa jinsi hiyo mteule wa MUNGU hatakiwi kutawaliwa nguvu za kiumbe yeyote duniani anayetumika kishetani.

Mkristo hutakiwi kutawaliwa na chochote cha kipepo.


Sasa ili wewe Mteule usitawaliwe ni lazima ujue njia ya kushinda vita ya kiroho.

Safari ya wokovu ni ya kushindana.

Ni lazima tushinde falme zote za giza.

Baadhi ya Kanuni za kiroho ili tushinde falme za giza;


1. Ni lazima ujue ROHO MTAKATIFU yupo na ni lazima ujazwe nguvu za ROHO MTAKATIFU.

-Huwezi kupigana vita ambayo humuoni adui hivyo Watu wa MUNGU tunamhitaji ROHO MTAKATIFU ili atujulishe ndipo tutashinda kila vita ya kiroho katika ulimwengu wa roho.

ROHO MTAKATIFU hutupa pia kupambanua.


1 Kor 12:3 ''3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika ROHO wa MUNGU, kusema, YESU amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, YESU ni Bwana, isipokuwa katika ROHO MTAKATIFU ''


3. Ni lazima ulijue Neno la MUNGU na ujue kulitumia ili kuwashinda mawakala wa shetani.

 

Ufunuo 12:11 '' Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. ''


 

 Mkristo ukitaka umiliki na kutawala katika ulimwengu wa roho inakupasa kuhusika na yafuatayo:-


1. Kuishi maisha matakatifu.

2. Kuomba katika ROHO MTAKATIFU.

3. Kuliishi kusudi la MUNGU na kumtumikia KRISTO.

4. Kufuata ufunuo wa maongozi ya ROHO MTAKATIFU.

5. Kumwamini MUNGU na kuziamini kazi zake kwa Kanisa.

6. Kujua kupigana vita ya kiroho.

7. Kujitenga na dhambi na machukizo yote ya dunia.


Kwa kufuata kanuni hizo zote saba hakika lazima umiliki na kutawala katika ulimwengu wa roho.

Waisraeli kama wateule wa MUNGU walipewa kumiliki.


Kumbu 9:1-4 " Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita wewe, miji mikubwa iliyojengewa kuta hata mbinguni, watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki?


 Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.


Usiseme moyoni mwako, BWANA, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia BWANA niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya BWANA awafukuza nje mbele yako."


Mataifa makubwa yenye nguvu ambayo hayatakiwi kuwa na nguvu mbele za Mkristo ni pamoja na wachawi wote, waganga, wakuu wa Giza wote, washirikina wote na kila mamlaka ya kipepo.


Hao unatakiwa uwatawale na sio wakutawale.


Unatakiwa wasiwe na nguvu juu yako, huko ndiko kuwamiliki na kutawala katika ulimwengu wa roho.


Inakupasa umiliki uzima na afya njema.


MUNGU anataka umiliki na kutawala.


Wachawi kama taifa kubwa lakini kwa Mteule wa KRISTO anayejitambua  hakika wachawi watapigwa na uchawi wao hautafanya kazi.


Teka waganga ili wakuondoe katika list ya watu wa kuonewa kipepo.


Mteule lazima umiliki na kuwatawala mataifa makubwa.

Inawezekana kuumwa kila mara ndio taifa kubwa linalokutesa.


Inawezekana kufungwa kipepo ili usipate kazi au usipate Mchumba ndio taifa kubwa linalokutesa, ndugu unatakiwa mataifa yako makubwa wasiwe na nguvu.

UBARIKIWE NA BWANA🙏

Comments

Popular posts from this blog

Pasaka/Easter✝️✅

CHRISTIAN RELATIONS BEFORE MARRIAGE💍💌