MAOMBI YA TOBA NA REHEMA

MAOMBI YA TOBA NA REHEMA

πŸ“– Zaburi 51:1–2

“Ee Mungu, unirehemu sawasawa na fadhili zako;

Kwa wingi wa rehema zako, uyafute makosa yangu.

Unioshe kabisa na uovu wangu,

Unitakase dhambi zangu.”


MAOMBI YA TOBA NA REHEMA🧎

Ee Baba wa mbinguni,

Nakuja mbele zako kwa unyenyekevu mkubwa, nikiwa na moyo wa toba.


Bwana, nakuomba unirehemu sawasawa na wingi wa fadhili zako.

Nisamehe dhambi zangu zote — nilizozifanya kwa kujua na hata zile nilizozifanya bila kujua.


Ee Mungu wangu,

yamkini kuna mlango niliufungua kwa njia ya dhambi,

mlango uliompa nafasi adui kuingia katika maisha yangu.

Kwa jina la Yesu,

ninatubu leo kwa dhati.


Naomba unioshe kwa damu ya Yesu, unitakase kabisa na uovu wangu.

Bwana,

kila mahali nilipokosea, kila hatua niliyopotoka,

naomba rehema zako zifute hatia yangu.


Ee Mungu,

ikiwa shetani ametumia udhaifu wangu kunirudisha nyuma,

hasa kupitia ndoto za shule, kunizuia nisipige hatua,

leo nasimama kinyume na hilo.

Kwa mamlaka ya jina la Yesu,

ninafunga kila mlango wa dhambi niliouwahi kufungua.

Ninavunja kila kifungo cha kiroho kinachonirudisha nyuma.


Kila ndoto ya kurudi nyuma,

kila ndoto ya mikwamo

naikataa sasa!

Bwana,

nirudishie nguvu,

nirudishie mwelekeo,

na unipe mwanzo mpya.

Ninapokea rehema zako,

ninapokea msamaha wako,

na ninatangaza kuwa nimewekwa huru.

Asante Baba kwa kunisamehe,

Asante kwa kunitakasa,

Asante kwa kunipa ushindi.

Katika jina la Yesu nimeomba,

AMEN.

JE, UNAJUA KWAMBA UNAPASWA KUOMBA KILA SIKU?

1. Kusali bila kukoma

1 Wathesalonike 5:17

“Ombeni bila kukoma.”

πŸ‘‰ Hii ina maana:

Maombi si ya siku moja tu

Ni ya kila wakati / kila siku

2. Yesu mwenyewe alifundisha kusali daima

Luka 18:1

“Akawaambia mfano ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.”

πŸ‘‰ Hapa Yesu anasisitiza:

Kusali sikuzote (kila wakati)

3. Kusali kila wakati kwa Roho

Waefeso 6:18

“Kwa sala zote na kuomba, mkisali kila wakati katika Roho…”

πŸ‘‰ Maana yake:

Hakuna muda maalum tu

Ni maisha ya maombi ya kila siku

4. Mfano wa watu wa Mungu waliosali kila siku

Zaburi 55:17

“Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalamika na kuugua; naye atasikia sauti yangu.”

πŸ‘‰ Hii inaonyesha:

Maombi ya mara kwa mara kila siku

5. Mfano wa Danieli

Danieli 6:10

“Akapiga magoti mara tatu kila siku, akaomba…”

πŸ‘‰ Mtu wa Mungu alikuwa:

Anasali kila siku bila kuacha

Hitimisho la maandiko

Kwa mujibu wa Biblia:

“Ombeni bila kukoma” (1 Wathesalonike 5:17)

“Mwombe Mungu sikuzote” (Luka 18:1)

“Mkisali kila wakati” (Waefeso 6:18)

πŸ‘‰ Ndiyo — Biblia inatufundisha tusali kila siku na hata kila wakati.


 HITIMISHO

BAADA ya Kuomba Kaa Kimya hata kwa dakika chache, ruhusu Roho Mtakatifu akuguse na kukujaza upya. Leo umeanza upya — na hakuna kitakachokurudisha nyuma tena.

FollowπŸ™

Comments

Popular posts from this blog

Choose Wisely+

BARAKA ZA BWANA