Waimbaji Hatupendani🫣

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Bella Kombo, amefunguka kuhusu uwepo wa matabaka, unafiki na ukosefu wa upendo miongoni mwa waimbaji wa muziki wa Injili nchini. 

Akizungumza kupitia Wasafi Media, Bella amesema baadhi ya wasanii wamejijengea makundi na kila mmoja kuwa na “ufalme wake”, hali inayodhoofisha ushirikiano katika tasnia hiyo. 

Ameeleza kuwa aliwahi kuchukua hatua ya kuwakutanisha waimbaji hao kufanya ibada ya pamoja, akiwahimiza kushirikiana, kusameheana na kutambua kuwa wote wanahudumia lengo moja, lakini bado changamoto hiyo imeendelea kujitokeza. 

Aidha, amesema hali hiyo imefikia hatua ya kushangaza hata waimbaji wa Injili kutoka mataifa mengine, wanaohoji ukosefu wa mshikamano miongoni mwa wasanii wa Tanzania.

Kuhusu sintofahamu iliyowahi kutokea kati yake na Joel Lwaga hadi kufikia hatua ya wawili hao kuitwa BASATA, Bella amefafanua kuwa ilitokana na mkanganyiko wa ratiba za matukio yao, huku akisisitiza kuwa kwa sasa hakuna tofauti kati yao na wanaendelea vizuri 

Follow for More

Comments

Popular posts from this blog

BARAKA ZA BWANA

Pasaka/Easter✝️✅

CHRISTIAN RELATIONS BEFORE MARRIAGE💍💌