Kwanini Hufanikiwi?

UKIANZA HII MICHEZO SAHAU KUFANIKIWA

1. πŸ“² mikopo ya Online

Hizi sio kausha damu tu, zinakausha mpaka Akili..

pesa inaingia sawa, lakini gharama yake ni kubwa kuliko unavyofikiria.

Riba zake zinakula mfuko wako kimya kimya, unakuja kushtuka unaishi kulipa madeni badala ya kujenga maisha.

2. Salary Advance

Kukopa mshahara wako kabla hujaufanyia kazi, unajifunga pingu mwenyewe.

Kila mwezi unaanza tayari ukiwa na madeni, unaanza ukiwa nyuma kifedha, akili yako haifikirii maendeleo bali namna ya kuziba mashimo.

3. 🎰 Betting

Najua hapa Utapiga tu..

Ukianza kutegemea betting kufanikiwa, akili yako inaacha kufikiria kimfumo.

Unaacha kujenga chanzo cha kipato, unaanza kusubiri ushindi wa bahati ambao mara nyingi hauji.

4. 🌐 Crypto Hype & Ponzi

95% nyingi ni utapeli tu unauziwa matumaini ya kuwa tajiri siku moja.

Hizi ni ahadi nzuri sana, zinaonekana kama shortcut ya utajiri. Wanakuonyesha maisha ya Dubai, lakini wanakuficha ukweli kuwa wengi wanaoingia mwisho wana hatari za kupoteza pesa zao.

5. πŸ™ Kutegemea watu (uchawa wa pesa)

Ukizoea kupewa, uwezo wako wa kujitengenezea unapotea. Unaacha kuwa creator wa maisha yako, unakuwa mtegemezi wa mood za watu wengine.

6. πŸ“± Fake Lifestyle

Unataka kuonekana una maisha makubwa kuliko kipato chako.

Unanunua vitu vya ku-impress watu ambao hata hawajali sana mwisho wake unajikuta umejaa madeni na stress

7. ⏳ Kuahirisha maisha (Procrastination)

Unaendelea kusema “bado muda upo” lakini ukweli ni huu, muda hauko upande wako. Miaka inapita haraka sana, na siku unakuja kushtuka unahitaji kuanza upya wakati ungekua mbali.

Ukiingia kwenye hizi michezo, sio kwamba unacheza — unaharibu mfumo wako wa maisha polepole bila kujua.

Maisha yanahitaji mtu anayechagua njia ngumu mapema ili aishi maisha rahisi baadaye.

Michezo gani hapa huwezi kuifanya?


Comments

Popular posts from this blog

BARAKA ZA BWANA

Pasaka/Easter✝️✅

CHRISTIAN RELATIONS BEFORE MARRIAGEπŸ’πŸ’Œ