Uzuri Wa Mazoezi Yakukimbia

FAIDA 4 ZA KIAFYA ZA KUFANYA MAZOEZI YA KUKIMBIA.

1. Huimarisha kinga dhidi ya magonjwa

 Utafiti unaonyesha  kwamba zoezi la kukimbia humsaidia mtu kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama vile mshtuko, kisukari na presha ya kushuka. Kwa kufanya zoezi la kukimbia mtu huimarisha kinga ya mwili wake na pia hufanyisha mazoezi misuli ya moyo na mishipa yake na hivyo basi kupunguza uwezekano wa maradhi ya moyo

  2. Husaidia kupunguza uzito na unene

   Swala la kupunguza unene wa mwili ni kati ya maswala ambayo huwatesa sana watu na mda mwingine hupelekea mtu kuchukua atua kama vile opareshen ya kutoa mafuta(contouring). Kutokana na utafiti unaonyesha kuwa zoezi la kukimbia ni kati za mazoezi yanayopunguza sana unene na kumfanya mtu kuwa na mwili mzuri wa mazoezi, basi inashauriwa mtu kufanya zoezi hili angalau mara tatu kwa wiki.

  3. Husaidia kupnguza msongo wa mawazo

 Kutokana na pilikapilika za kila siku za maisha msongo wa mawazo ni kitu cha kawaida kumpata mtu yeyote. Utafiti unaonyesha yakwamba  kwa kufanya zoezi la kukimbia mtu anaweza kuufanya mwili wake kuweza kuzalisha homoni zenye tija na hivyo kutumia nguvu nyingi ambapo hupunguza uwezekano wa msongo wa mawazo.

4 Husaidia uimarishaji wa mifupa na misuli

 Zoezi la kukimbia husaidia mwili sana hasa kwenye ukazaji na uhimarishaji wa mifupa na misuli. Kulingana na utafiti uliofanywa Dr brok unaonyesha ya kwamba mtu anavyozidi kukimbia na umri wake unavyozidi kuongezeka ndivyo anavyo himarika zaidi kwenye misuli na mifupa yake.

VIPIMO KABLA YA KUKIMBIA

Kumbuka kabla ya kutaka kufanya mazoezi ya kukimbia ni vyema mtu kumwona daktari kwa ushauri  na vipimo vya afya yake. 

VIFAA VYA MAZOEZI YA KUKIMBIA

Mtu anayetaka kufanya mazoezi ya kukimbia analazimika kutafuta:-

Nguo nyepesi kama 

(bukta ama traksuti  na pia kutafuta viatu vyepesi vya kukimbilia mfano raba).

Comments

Popular posts from this blog

BARAKA ZA BWANA

Pasaka/Easter✝️✅

CHRISTIAN RELATIONS BEFORE MARRIAGE๐Ÿ’๐Ÿ’Œ