BARAKA ZA BWANA
POKEA BARAKA ZA BWANA Kuna aina tano(5) za baraka atoazo MUNGU kwa watu wake. 1. Baraka za afya. 2. Baraka za uchumi. 3. Baraka za ndoa. 4. Baraka za uzao. 5. Baraka za kutamalaki. Baraka yake kutamalaki kwa jina lingine inaitwa Kumiliki na kutawala, Sasa moja ya mamlaka ya Mteule wa MUNGU aliyeokolewa na Bwana YESU ni kumiliki na kutawala kwenye ulimwengu wa roho. Tunamiliki na kutawala kwa sababu tuna mamlaka ya jina la YESU KRISTO. Jukumu la kwanza tulilopewa wanadamu na MUNGU Muumba wetu ni kutawala. Mwanzo 1:26-27 ''MUNGU akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; WAKATAWALE samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba'' Kwa jinsi hiyo mteule wa MUNGU hatakiwi kutawaliwa nguvu za kiumbe yeyote duniani anayetumika kishetani. Mkristo hutakiwi kutawaliwa na chochote cha kipepo. Sasa il...

Comments
Post a Comment